Wahanga wa janga la njaa wahitaji msaada zaidi
25 Septemba 2011Matangazo
Katibu Mkuu Ban, alipozungumza mjini New York, alisema, katika kipindi cha mwaka mmoja pekee, kunahitajiwa msaada mwingine wa dola milioni 700 ili kuweza kuokoa maisha ya watu milioni 13 walioathirika nchini Somalia, Kenya na Ethiopia.
Wakati huo huo, Benki ya Dunia imearifu kuwa itaongeza msaada wake hadi kufikia takriban dola bilioni 1 nukta 9.