1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri waitaka Ujerumani iingilie Mashariki ya Kati

Abdu Said Mtullya9 Julai 2014

Wahariri leo wanazungumzia juu ya mgogoro wa Mashariki ya Kati, na bila shaka juu ya ushindi wa timu ya Ujerumani katika nusu fainali ya kombe la Dunia.

https://p.dw.com/p/1CYf5
Ukanda wa Gaza wawaka moto
Ukanda wa Gaza wawaka motoPicha: Reuters

Hali imezidi kupambana moto.Ndege za Israel zimefanya mashambulio mengi na watu kadhaa wameshuawa katika Ukanda wa Gaza. Mhariri wa gazeti la "Berliner Morgenpost" anaitaka Ujerumani ilichukue jukumu maalamu katika ,kuuondosha mvutano ili Israel na Wapalestina wautatue mgogoro wao kwa njia ya mazungumzo.

Mhariri wa "Berliner Morgenpost" anesena Ujerumani inapaswa kulitekeleza jukumu hilo maalumu kwa sababu usalama wa Israel ni sehemu ya sera ya msingi ya Ujerumani.

Hamas yasimama peke yake
Gazeti la "Nordwest" pia linauzungumzia mgogoro wa Mashariki ya Kati kwa kuutilia maanani uhusiano baina ya Hamas na Misri.

Gazeti hilo linasema Hamas sasa imesimama peke yake. Nchini Misri watawala siyo tena wale wanaotoka katika jumuiya ya Udugu wa kiislamu waliokuwa wanawaunga mkono Hamas . Njia za chini ya ardhi ambazo Hamas walikuwa wanazitumia ili kupenyezea silaha sasa zimezibwa. Aidha chama cha Hamas kinaishiwa fedha. Ni katika hali hiyo kwamba Hamas imeimarisha mashambulio dhidi ya Israel-lengo ni kuyatumia mapambano na Israel ili watu wa Ukanda wa Gaza wayasahau matatizo ya ndani.

Na mhariri gazeti "Bild Zeitung"anasema vita vimekuwa kama jambo la kawaida katika Mashariki ya Kati.Ni mgogoro wa hatari, lakini adui mkubwa ni utepetevu wa nchi za magharibi!

Magharibi isaidie kujenga miundo mbinu ya demokrasia Afghanistan

Mhariri wa gazeti la "Frankfurter Rundschau" anazitaka nchi za magharibi ziweke mkazo katika maendeleo ya kijamii nchini Afghanistan, la sivyo nchi hiyo itarudi kule kule ilikotoka-katika vurumai. Mhariri wa gazeti hilo anasema wachunguzi wengi katika nchi za magharibi wanasema kuwa watu wa Afghanistan hawaijui demokrasia.

Hatahivyo wanaosema hivyo wanapaswa kukumbuka kwamba nchi za magharibi ziliingia Afghanistan kijeshi ili kupambana na magaidi wa Taliban.Lakini kabla ya hapo hakuna aliejua juu ya kazi kubwa ya kuijenga upya nchi hiyo. Baada ya harakati za kijeshi zilizoongozwa na Marekani sasa nchi za magharibi zinapaswa kuweka mkazo katika kuijenga miundo mbinu ya demokrasia nchini Afghanistan na hivyo kuujenga usalama , la sivyo nchi hiyo itarudi ilikotokea-.

Brazil yapata kipigo
Hakuna alieyaamini macho yake kwani kilikuwa kama kiini macho! Brazil ilielibeba kombe la dunia mara tano jana iliadhiriwa na timu ya Ujerumani baada ya kuchabangwa mabao saba kwa moja. Gazeti la "Kölner Stadt Anzeiger" linasema anaeshinda siyo lazima awe hodari zaidi. Refa anaweza kuyatibua mambo.Au timu nzuri inaweza kukumbwa na bahati mbaya. Lakini baada ya ushindi wa jana timu ya Ujerumani inaweza kuwa na matumaini ya kulibeba kombe-sababu timu hiyo ,ni kitu kimoja na siyo mtu mmoja. Timu ya Ujerumani na mikakati imara na wachezaji wake pia ni imara.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman