1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe wa ECOWAS wawasili Cote d'Ivoire

28 Desemba 2010

Marais wa Benin, Sierra Leone na Cape Verde wamewasili Abidjan, mji mkuu wa Cote d'Ivoire katika jitahada ya kumshawishi Rais Laurent Gbagbo kuondoka madarakani au kukabiliwa na nguvu za kijeshi.

https://p.dw.com/p/QklO
Ivory Coast, President Laurent Gbagbo, Speak during an exclusive interview at his residence, in Abidjan, Sunday, Dec. 26, 2010. West African leaders are giving the man who refuses to leave Ivory Coast's presidency a final chance to hand over power and are threatening to remove him by force if needed, though doubts exist about whether the operation could be carried out. (AP Photo/Sunday Alamba)
Rais Laurent Gbagbo wa Cote d'Ivoire anaeshinikizwa kungátuka madarakani.Picha: AP

Marais Bon Yayi wa Benin, Ernest Koroma wa Sierra Leone na Pedro Pires wa Cape Verde wamepelekwa Abidjan na Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi-ECOWAS kumuonya Gbagbo kuwa vikosi vya kanda hiyo huenda vikapelekwa Cote d'Ivoire kumngóa madarakani akiendelea na ubishi wake.Kwa kweli, marais hao watatu si miongoni mwa wakosoaji wakubwa wa Gbagbo katika ECOWAS, lakini wamekwenda na ujumbe uliotiwa saini na viongozi wenye usemi zaidi kama vile Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria, ukimtaka kiongozi huyo angátuke madarakani.

Hata hivyo, hakuna ishara kuwa Gbagbo atauitikia wito huo kwani anaenedelea kushikilia kuwa yeye ndie aliechaguliwa kihalali kuwa kiongozi wa Cote d'Ivoire. Vile vile ameonya kuwa kitisho cha kutumia nguvu za kijeshi za ECOWAS huenda kikazusha vita katika kanda hiyo ya Afrika Magharibi.

Hapo awali, Waziri wa Mambo ya Ndani Emile Guirieoulou alisema kuwa wajumbe wa ECOWAS watakaribishwa kama ndugu na marafiki lakini wanapaswa kuheshimu uhuru wa Cote d'Ivoire. Serikali haitovumilia mambo yake kuingiliwa kati wala haitoitikia mwito wo wote ule wa kumkabidhi madaraka Ouattara. Msemaji wa serikali Ahoua Don Melo amesema, hakuna taasisi yo yote ile ya kimataifa iliyo na haki ya kuingilia kati na kumweka rais katika nchi inayojitawala yenyewe.

Opposition leader Alassane Ouattara addresses the press at a news conference at Golf Hotel in Abidjan, Ivory Coast, Wednesday, Dec. 1, 2010. With only hours to go before the midnight deadline for the release of Ivory Coast's provisional election results, the electoral commission remained deadlocked Wednesday as the country's ruling party continued to prevent the issuance of partial results.(AP Photo/Rebecca Blackwell)
Alassane Ouattara atambuliwa na ECOWAS mshindi wa uchaguzi wa rais Cote d'Ivoire.Picha: AP

Wote Gbagbo na Ouattara wanadai kushinda uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita na kila mmoja wao amejitangaza rais.Lakini Ouattara ndie alietambuliwa na wasimamizi wa uchaguzi wa Umoja wa Mataifa na madola makuu kama mshindi wa uchaguzi huo wa rais. Ouattara anaeitumia hoteli moja mjini Abidjan, kama makao yake makuu analindwa na vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa kwani amezingirwa na wanajeshi wanaomuunga mkono Gbagbo.

Zaidi ya watu 170 wameuawa katika machafuko yaliyozuka nchini humo kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita. Inahofiwa kuwa nchi hiyo ipo katika hatari ya kurejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwandishi.P.Martin/AFPE/RTRE

Mpitiaji:Josephat Charo