1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakaazi waliopewa hifadhi kwenye kambi za muda nchini Kenya warejeshwa makwao

5 Mei 2008

Nchini Kenya operesheni ya kitaifa ya kuwarejesha makwao wakaazi waliokuwa wakipewa hifadhi kwenye kambi za muda katika mkoa wa Bonde la Ufa imeanza rasmi hii leo.

https://p.dw.com/p/DtvS
Watu waliolazimika kuyahama makaazi yao baada ya vurugu za Uchaguzi nchini KenyaPicha: Picture-Alliance /dpa

Taarifa zinaeleza kuwa kumeundwa vituo 32 vya polisi kwa lengo la kudumisha usalama katika eneo hilo.Hatua hii inachukuliwa baada ya Rais Mwai Kibaki na waziri Mkuu Raila Odinga wote wakiandamana na Makamu wa Rais kuzuru eneo hilo mwishoni mwa mwezi uliopita.Hata hivyo baadhi ya waathirika wa ghasia za uchaguzi pamoja na wanaharakati na viongozi wa kidini hatua ya maridhiano ingepewa kipaumbele na kujumuisha wahusika wote.

Kutoka Nairobi Mwai Gikonyo anaarifu zaidi.