1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakenya waamua leo, kukubali ama kukataa katiba mpya.

Halima Nyanza4 Agosti 2010

Wananchi wa Kenya leo wanapiga kura ya maoni juu ya kuikubali au kuipinga katiba mpya ya nchi yao.

https://p.dw.com/p/ObRB
Zoezi la upigaji kura likiendelea leo nchini Kenya.Picha: AP

Katiba hiyo mpya ni sehemu ya mpango wa mabadiliko unaonuia kuzuwia kutokea tena vurugu  katika uchaguzi mwingine mwaka 2012.

Jana Tume hiyo ya uchaguzi ilieleza kuwa haitarajii kutokea tena vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2007, wakati wa zoezi hilo la leo la upigaji kura.

Ulinzi waimarishwa:

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume huru ya muda ya uchaguzi nchini Kenya, Ahmed Issack Hassan, usalama umeimarishwa katika maeneo yanayohofiwa kuzuka vurugu ambapo maafisa zaidi wa polisi wamesambazwa katika maeneo hayo.

Kenia Wahl Nairobi
Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.Picha: AP

Kura hiyo ya maoni ni ya kwanza kupigwa kitaifa baada ya uchaguzi huo mkuu uliosababisha vurugu na mauaji ya zaidi ya watu 1,300.