1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakenya washinda New York marathon

4 Novemba 2014

Wilson Kipsang ameshinda mbio za marathon za mjini New York na mwenzake kutoka Kenya Mary Keitany amenyakua ushindi wa mbio hizo kwa upande wa wanawake.

https://p.dw.com/p/1DgiM
New York City Marathon 03.11.2013
Picha: Getty Images

Kipsang ameshinda kwa saa mbili dakika 10 na sekunde 55 na kupata kitita cha dola100,000. Dennis Kimetho pia kutoka Kenya alikuwa wa pili.

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC imesifu azimio la Umoja wa mataifa kutambua uhuru wa michezo kuwa ni chombo muhimu ambacho kitasaidia kuweka hali ya kujitenga na siasa pamoja na kusababisha nchi kususia michezo pamoja na ubaguzi.

Azimio lililoidhinishwa na baraza kuu la Umoja wa mataifa linaeleza kuwa Umoja huo unaunga mkono uhuru na mamlaka ya michezo pamoja na ujumbe wa IOC katika kuongoza shirikisho hilo la Olimpiki.

Na wakaguzi kutoka shirikisho la michezo ya riadha IAAF wametembelea miji mitatu inayowania kuwa wenyeji wa michezo ya duinia ya riadha mwaka 2019, ambapo Barcelona, Doha na Eugene yote ikiwa na uwezo wa kutayarisha michezo hiyo kwa hali bora kabisa.

Mwandishi : Sekione Kitojo / dpae / rtre / afpe / zr
Mhariri : Mohammed Abdul Rahman