1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakili akosoa hatua ya polisi kuhusu sakata la viongozi wa gazeti la Standard nchini Kenya

17 Aprili 2007

Hatua ya maafisa wa usalama kuwatia nguvuni na kuwahoji kwa masaa 6 viongozi wa gazeti la The Standard nchini Kenya,baada ya kuandika makala ya mahojiano na mmoja kati ya ndugu wawili wanaojulikana kama "KINA ARTUR" wenye asili ya Armenia na waliogonga vichwa vya habari kwa muda mrefu sasa, imekosolewa kuanzia na wanasiasa wa upinzani, waandishi habari na hata mawakili.

https://p.dw.com/p/CHG7

Kwa mujibu wa habari hizo, Artur Magarian alidai kwamba alitakiwa na waziri mmoja wa ngazi ya juu kuchunguza akaunti za mbunge Gideon Moi, mtoto wa Rais wa zamani Daniel Arap Moi huko Dubai na kuandaa mpango wa kumteka nyara. Gazeti hilo liliwasilisha polisi kanda za mahojiano hayo kama ushahidi. Je hatua ya polisi kuwatia nguvuni na kutaka viongozi wa gazeti hilo watoe ushahidi ilikuwa ni ya halali?

Mohamed Abdulrahman alizungumza na mwanasheria Harun Ndubi kwa njia ya simu akiwa mjini Nairobi ambaye kwanza alikuwa na haya ya kueleza.