1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

140110 Kambodscha Vergangenheitsbewältigung

Josephat Nyiro Charo20 Januari 2010

Kesi kusikilizwa katika mahakama ya Umoja wa Mataifa

https://p.dw.com/p/Lbya
Kamanda wa gereza la Khmer Rouge Kaing Guek Eav (kulia) anayejulika pia kama "Duch"Picha: AP

Chini ya utawala wa kidikteta wa Pol Pot na Khmer Rougue nchini Cambodia kati ya mwaka 1975 na 1979 watu milioni mbili waliuwawa. Miaka 30 tangu mauaji hayo kufanyika kesi dhidi ya matukio ya enzi hiyo imeshika kasi. Wakili mwanamke wa Ujerumani anasimama kizimbani kwa niaba ya wahanga wa mauaji hayo.

Mnamo mwaka 2008 idara ya ushirikiano wa kimaendeleo ya Ujerumani mjini Berlin ilimtuma wakili mwanamke Silke Studzinsky kufanya kazi ya kiraia katika juhudi za kudumisha amani huko Phnom Penh, Cambodia. Huko Studzinsky anawawakilisha wahanga wa mauaji yaliyofanywa wakati wa utawala wa chama cha kikomunisti cha Cambodia, mbele ya mahakama maalum inayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa.

Kuna mambo kadhaa ambayo tayari amefaulu kuyafanikisha. Bila yeye wafuasi wa chama hicho wangeendelea kufanya ubakaji kwa mfano kupitia idadi kubwa ya ndoa za lazima. Kiwango cha mauaji na mateso yaliyofanywa na chama cha kikomunisti nchini Cambodia ni mambo yaliyomsukuma Silke Studzinsky kujishughulisha na kesi hiyo kama anavyoeleza.

"Wafuasi wa chama cha kikomunisti cha Cambodia waliua, walitesa lakini walipopatikana na makosa ya ubakaji waliadhibiwa vikali. Hivi ndivyo historia ilivyoendelezwa na wanahistoria wanaume."

Wakati wakili Silke Studzinsky alipowasili nchini Cambodia, hakuwa na uzoefu lakini kupitia kazi yake ya hapo awali kama wakili, aliguswa sana na swala la ubakaji. Silke amesema hapo zamani watu nchini Cambodia walilazimishwa kuingia katika ndoa. Hakuna aliyeuliza na hata ukiuliza hakuna jibu lililotolewa, hakuna haki hata katika swala kama hili.

Katika kesi dhidi ya mshukiwa wa kwanza Kaing Guek Eav anayejulikana pia kama Duch swala hili liligusiwa kidogo mwishoni mwa mchakato wa kusikilizwa kesi hiyo. Kesi hiyo dhidi ya Duch katika mahakama hiyo maalum ya Umoja wa Mataifa, ilikuwa afueni kubwa amethibitisha Studzinsky. Lakini hata hivyo anakosoa maovu yaliyofanywa na utawala wa kigaidi wa Cambodia.

"Ni jambo la kawaida hapa kwamba karibu kila mtu anajihisi kamamhanga. Na kwa hivyo jukumu la kuwa muhanga si la kulia shaka miongoni mwa kizazi kipya. Pol Pot ndiyo aliyekuwa mtu pekee aliyetoa amri na wengine wote walilazimika kumtii la sivyo wao wenyewe wangeuwawa. Hilo ni jukumu la muhanga ambalo watu wote walioshi wakati huo wamo ndani."

Duch amejitetea akisema hata yeye mwenyewe hakuwa na chaguo lengine. Juu ya hayo mawakili wake wamelalamikia jinsi mteja wao anavyoshughulikiwa na hukumu itakayotolewa dhidi yake. Duch amechaguliwa kama kondoo wa sadaka huku magaidi wengine wabaya zaidi wakiendelea kujificha. Silke Studzinsky amekiri kwamba orodha ya washukiwa ni ndefu lakini Duch hawezi kuwataja.

Baada ya kusikilizwa kesi dhidi ya Duch kesi ya washukiwa wengine wanne nayo itasikiliwa. Wakati huo huo kesi ya washukiwa wengine watano ambao hawakuwa watu mashuhuri sana wakati wa utawala wa chama cha kikomunisti cha Cambodia imeanza kusikilizwa. Washukiwa wengine zaidi wanatarajiwa kukamatwa. Silke Studzinsky anawawakilisha wahanga wa mauaji ya Cambodia katika mahakama hiyo maalum ya Umoja wa Mataifa. Amerefusha mkataba wake kwa kipindi kifupi hadi mwishoni mwa mwaka huu 2010.

Mwandishi: Thomas Betlein/ZPR

Mhariri: Aboubakary Liongo