1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi wa Kinyarwanda nchini Uganda warejea nchini mwao

13 Mei 2009

Kundi la kwanza la wakimbizi 20,000 wa Kinyarwanda waishio nchini Uganda limevuka mpaka kurejea nchini mwao.

https://p.dw.com/p/HpUb
Wakimbizi wa KinyarwandaPicha: AP

Kundi hilo la wakimbizi 80 lilivuka mpaka jana jioni kwenye kituo cha Katuna, na wote wanatarajiwa kupelekwa kwenye vijiji walikotoka. Kurejea nyumbani kwa wakimbizi hao kunafuatia makubaliano kati ya serikali za Rwanda na Uganda, kwamba ifikapo tarehe 31 mwezi Julai mwaka huu, wakimbizi wa Rwanda watakaobakia kwenye ardhi ya Uganda watachukuliwa kama wahamiaji haramu.

Mwandishi wetu mjini Kiagali Daniel Gakuba ana maelezo zaidi.


Mwandishi: Daniel Gakuba

Mhariri: Mohamed Abdulrahman