1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakulima wadogo wadogo kuwezeshwa kikazi

Mohamed Abdulrahman18 Oktoba 2013

Mpango wa Shirika la FAO, unatafuta juhudi za hivi sasa za kupata usalama wa chakula, Badala ya kuzingatia hasa uzalishaji chakula unaangazia kuzigeuza bidhaa ndogo ndogo za kilimo kuwa za kibiashara.

https://p.dw.com/p/1A2DS
Nembo ya FAO
Nembo ya FAOPicha: AP Graphics

Miaka sita tangu mpango huo uanze kufanya kazi, ufadhili na kupunguzwa kwa matumizi ni mambo yaliovuruga mustakbali wa mapngo huo, licha ya kwamba Shirika la kilimo na chakula duniani -FAOna lile la ushirikiano wa maendeleo la Italia ambalo ni mfadhili wa mpango huo wa kilimo cha biashara zinatathmini maendeleo yaliopatikana.

Naibu mkurugenzi mkuu wa FAO alisema wakati wa kuadhimishwa wiki ya chakula hivi karibuni katika makao maku ya Shirika hilo mjini Roma, kwamba hata kama tunataka kuishinda njaa kuongeza uzalishaji si jambo linalotosha kukabiliana na changamoto za soko la chakula duniani.

Katika kila eneo miongoni mwa kanda nne zinazohusika na mpango wa kilimo cha bidhaa ndogo ndogo kuwa za kibiashara, nchi husika zilitekeleza mpango huo kulingana na mahitaji yao. Kanda hizo ni Amerika kati, Afrika mashariki, Afrika magharibi na Karibik.

Zao la Mahindi
Zao la MahindiPicha: UN Photo / BZ

Mousa Djagoudi kutoka ofisi ndogo ya FAo katika Afrika Magharibi alifafanua katika hotuba yake wakati wa sherehe nchini Sierra Leone kwamba fedaha zimetumika kujenga vituo 30 vya kilimo cha biashara ili kuboresha chakula na kupunguza hasara ya chakula na katika baadhi ya matukio, kufikia hadi 40 asili mia,.

Mpango huo umeweza kuboresha pia utumaji teknolojia kwa wakulima awadogo awadogo na kwamba leo wanaafahamu kuwa "Kilimo ni Biashara."

Wakati lengo la baadhi ya wakulima katika maeneo mengine ni kuyafikia masoko katika maeneo tajiri duniani huko kanda ya maziwa makuu barani Afrika , sisitizo kubwa ni katika miradi ya nchi hadi nchi pamoja na mahitaji ya watu katika kanda hiyo, alau kwa baadhi tu ya bidhaa.

Waziri wa kilimo wa Uganda aelezea hali ilivyo nchini humo

Waziri wa kilimo wa Uganda Bright (BRAIT)Rwamirama, anaeleza kwamba kieneo nchini Uganda, rwanda , Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zaidi ya watu 15,000 wamenufaika moja kwa moja kutokana na miradi hiyo ya kilimo kawa ajili ya biashara.

Pia ya bidhaa zililengwa masoko ya ndani, kwa mfano asali na nyengine kama mananasi na embe ambayo ni mazao yalionunuliwa ana kampuni za chakula na kuuzwa nchi za nje.

Mkuu wa FAO José Graziano da Silva
Mkuu wa FAO José Graziano da SilvaPicha: DW/R. Belincanta

Kwa mujibu wa Jorge Alberto Salina Rodriguez, mkurugenzi katika ofisi ya mipango na sera ,zaidi ya wakulima 600 walihusika katika mpango huo ambao umesaidia kuondoa upungufu wa chakula kutoka 20 asili mia hadi karibu 8 asili mia.

Wadadisi wanasema mpango huo wa klilimo cha mazao madogo kwa ajili ya biashara umezaa matunda kwa kiasi fulani kwa sababu serikali ziliwapuuza wakulima wadogo wadogo.

Lakini pamoja na hayo, yaliopatikana hayatoshi kutatua tatizo la umasikini katika maeneo ya vijijini.Juhudi za ziada zinahitajika kuongeza teknolojia kwa wakulima pamoja na nafasi katika masoko.Hayo ni amambo muhimu, hasa katika nchi ambako kilimo vijijini kilipuuzwa na serikali kwa miaka mingi.

Mwandishi: Sudi Mnette, IPS

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman