1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliofyetulia risasi polisi watafikishwa mahakamani

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUG7

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameapa kuchukua hatua dhidi ya wafanya ghasia waliyowafyetulia risasi askari polisi wakati wa maandamano ya machafuko,hasa katika vitongoji vya mji mkuu Paris.

Rais Sarkozy alierejea kutoka ziara yake ya China,aliwatembelea polisi waliojeruhiwa vibaya katika machafuko hayo.Ghasia hizo zilizuka siku ya Jumapili baada ya vijana 2 kufariki pale pikipiki yao ilipogongána na gari la polisi.Hadi polisi 120 wamejeruhiwa katika machafuko ya siku tatu.Hayo ni machafuko mabaya kabisa kutokea katika vitongoji vya Paris,tangu zile ghasia kubwa za mwaka 2005.