1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamnajeshi wa Uengereza waihama Basra

Oummilkheir16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcLE

Bassra:

Waengereza wamewakabidhi wairak hii leo hatamu za ulinzi katika jimbo tajiri kwa Mafuta-Basra.”Usalama wa Basra unadhibitiwa na wairak hivi sasa” amesema kwa fahari Muaffak al Rubei,mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Irak.Bwana Al Rubei ndie aliyemuakilisha waziri mkuu Nuri el Maliki katika sherehe za kukabidhiwa wairak dhamana ya ulinzi katika jimbo hilo la mwisho kati ya majimbo 4 yaliyokua yakisimamiwa na Uengereza.Mkuu wa vikosi vya Uengereza Graham Binns ametiliana saini waraka wa makubaliano pamoja na gavana wa Basra Mohammed al Waili,kuhusu kurejeshwa jimbo hilo lenye wakaazi milioni mbili na laki sita lililokua likikaliwa na wanajeshi wa Uengereza tangu March mwaka 2003.Jumla ya majimbo tisaa kati ya 18 ya Irak yanadhibitiwa upya hivi sasa na wenyewe wa Irak.Kwa mujibu wa utafiti wa maoni ya umma uliofanywa na kituo cha matángazo cha BBC huko Basra,asili mia 68 ya wairak hawakuridhishwa na kuwepo wanajeshi wa Uengereza katika eneo lao.