1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 2 wauawa wakitegua bomu Mogadishu

Daniel Gakuba
17 Mei 2017

Wanajeshi wawili wamepoteza maisha baada ya kutokea mripuko wa bomu la kutegwa ndani ya gari walipokuwa wakijaribu kulitegua bomu hilo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, hii leo.

https://p.dw.com/p/2d6Bz
Somalia Explosion vor einem Hotel in Mogadishu
Picha: picture-alliance/abaca/AA/A. M. Tuuryare

Kwa mujibu wa afisa wa poolisi Meja Nur Ahmed aliyezungumza na shirika la habari la Reuters, wanajeshi hao waliuwawa walipokuwa wakivunja sehemu ya gari na kisha  bomu hilo kuripuka.

Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika, ingawa wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab wameanzisha msururu wa mashambulizi mjini Mogadishu na maeneo mengine nje ya mji huo wakijaribu kulazimisha kuweka utaratibu wa sheria za Kiislamu.

Somalia iko katika vita tangu mwaka 1991 baada ya wababe wa kivita kumuangusha madarakani dikteta Siad Barre na baaday kugeukiana wenyewe kwa wenyewe.