1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshikamano wa kimataifa

12 Januari 2015

Mkutano wa usalama wa taifa unafanyika Elysée ,siku moja tu baada ya maandamano ya kihistoria mjini Paris na katika miji yote mengine ya Ufaransa kupinga mashamblio ya kigaidi yaliyoitumbukiza msibani Ufaransa.

https://p.dw.com/p/1EIpp
Maombolezi kuwakumbuka wahanga wa mashambulio mjini ParisPicha: AFP/Getty Images/G. Tibbon

Wakikabiliwa na kitisho kikubwa kabisa cha kutokea wimbi jengine la mashambulio,rais wa Ufaransa Francois Hollande amekutana na waziri mkuu Manuel Valls,waziri wa mambo ya ndani Bernard Caseneuve, na mwenzao wa sheria Christiane Taubira pamoja na wakuu wa idara za usalama katika kasri lake huko Elysée.

"Ufaransa bado inakabiliwa na vitisho" alionya hapo awali rais Hollande huku serikali yake ikiungama kumekuwa na "ufa" katika opereshini za usalama zilizoanzishwa katika nyanja tofauti dhidi ya wafuasi wa itikadi kali.

Wanajeshi 10 000 kusimamia usalama

Waziri mkuu Manuel Valls amesema kabla ya kuhudhuria mkutano wa usalama katika kasri la rais kwamba jumla ya wanajeshi 10 000 watawekwa katika kila pembe kuambatana na mpango madhubuti wa kupambana na ugaidi-"Vigipirate"-Akizungumza na kituo cha televisheni cha BFMTV waziri mkuu Manuel Valls amefafanua hatua za usalama zimeimarishwa kuliko wakati wowote ule mwengine.Wanajeshi 5000 wanawekwa kulinda masinagogi na shule za kiyahudi.Waziri mkuu Valls ameongeza kusema hata misikiti italindwa kutokana na mashambulio yaliyotokea hivi karibuni kufuatia mashambulio ya kigaidi yaliyoangamiza maisha ya watu wasiopungua 17 wiki liyopita.

Frankreich verstärkte Sicherheitsmaßnahmen 11.01.2015
Hatua za usalama zaimarishwaPicha: Getty Images/P. Aventurier

Jana umati wa watu, zaidi ya milioni tatu na nusu waliokuwa na nyuso za huzuni na furaha waliteremka majiani mjini Paris na katika kila pembe ya Ufaransa kuonyesha mshikamano na kulaani matumizi ya nguvu-maaandamano yaliyofanyika wakati mmoja na yale ya viongozi zaidi ya 50 wa kimataifa walioteremka pamoja na rais Francois Hollande hadi katika uwanjka mashuhuri wa Place de la Republik mjini Paris.

Zaidi ya watu milioni moja na nusu waliteremka mjini Paris kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndanmi Berard Caseneuve.

Maandamano hayo yalipangwa hapo awali kuwakumbuka wahanga wa mashambulio ya kigaidi wakiwemo wachoraji wa jarida la tashtiti la Charlie Hebdo waliouliwa jumatano iliyopita ,askari polisi mmoja wa tarafa aliyeuliwa alkhamis na wayahudi wannme waliouliwa ijumaa katika duka la kiyahudi-Casher ijumaa iliyopita.

Yalijipatia kipeo cha kimataifa na kutoa picha ya viongozi wa kimataifa waliokamatana mikono,nyuso zimekunjwa hadi katika uwanja wa Place de la Republique.Francois Hollande amezungukwa na kansela Angela Merkel,kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas,waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu,,waziri mku wa Uengereza David Cameon,mfalme wa Joradan,waziri mkuu wa Italy,tukiwataja kwa uchache.....

Mshikamano wa kimataifa dhidi ya ugaidi

Wakishangiriwa na umati wa watu walipowasili,viongozi hao wa kimataifa walisalia kimya dakika moja kabla ya kurejea kataika kasri la rais Elysée.Rais Hollande aliwaamkia familia za wahanga waliokuwa safu ya mbele ya maandamano hayo.

Paris Charlie Hebdo Terroranschlag Hommage Frankreich Trauer
Umati wa watu wasiojulikana idadi halisi,wakichanganyika na viongozi wa kimataifa katika uwanja wa Place de la Republique mjini ParisPicha: picture-alliance/dpa

Hisia za mshikamano ndizo zilizojitokeza.Meya wa jiji la kaskazini la Lille Martine Aubry anasema:"Nna furaha kuona umati mkubwa kama huu wa watu kutoka asili,tamaduni ,na umri na mirengo tofauti ya kisiasa waliosimama kidete kusema hatutaki ugaidi,.Kuwepo viongozi wa kimataifa kunabainisha haya ni mapambano ya kimataifa."

Wakati huo huo juhudi za kumsaka angalao mtuhumiwa mmoja anaesemekana huenda amewasaidia waasisi wa tatu wa mashambulio ya wiki iliyopita mjini Paris,zinaendelea.

Mwadishi:Hamidou Oummil/Reuters/AFP

Mhariri:Josephat Charo