1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Australia wamewasili Timor Mashariki

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6YQ
Wanajeshi wa Australia wameanza kuwasili nchini Timor Mashariki hii leo kusaidia kutekeleza amri ya hali ya hatari iliyotangazwa baada ya rais wa nchi hiyo kupigwa risadi hapo jana. Rais wa Timor Mashariki Jose Ramos Horta alijeruhiwa vibaya wakati alipopingwa risasi tumboni akiwa nyumbani kwake nje ya mji mkuu Dili. Baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya jeshi la Australia katikati mwa Dili rais Ramos Horta alipelekwa nchini Australia ambako anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Royal Darwin. Madaktari wanaomhudumia wamesema ataendelea kusaidiwa na mashine za kupumua hadi wikiijayo. Umoja wa Mataifa umesema watu 11 wamehojiwa kuhusiana na shambulio la jana ambapo mwanajeshi muasi aliuwawa. Wakati huo huo,kamanda mkuu wa jeshi la Timor Mashariki ametaka maelezo vipi wanajeshi waasi waliweza kuingia makazi ya rais na waziri mkuu kufanya mashambulio ya kutaka kuwaua. Brigedia jenerali Taur Matan Ruak amesema jeshi lina jukumu la kulinda usalama nje ya makaazi ya rais huku polisi ya nchi hiyo na polisi ya Umoja wa Mataifa ikiwa na kazi ya kumlinda rais.