1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wanane wa Marekani wauwawa

Mohamed Dahman10 Novemba 2007

Wanajeshi sita wa Marekani na watatu wa Afghanistan wameuwawa wakati waasi waliposhambulia msafara wao wa doria kwenye milima ya nyanda za juu mashariki mwa Afghanistan hilo likiwa ni shambulio baya kabisa dhidi ya vikosi vya Marekani mwaka huu.

https://p.dw.com/p/CH77
Wanajeshi wa Marekani wakiwa mbele ya gari la deraya katika mojawapo ya doria zao nchini Afghanistna.
Wanajeshi wa Marekani wakiwa mbele ya gari la deraya katika mojawapo ya doria zao nchini Afghanistna.Picha: AP

Wanajeshi hao walikuwa wakirudi kwenye mkutano na viongozi wa kijiji jana alasiri katika jimbo la Nuristan wakati wanamgambo walipowashambulia kwa maroketi na risasi.

Imeelezwa kwamba walishambuliwa kutoka sehemu kadhaa za maadui kwa wakati mmoja na kwamba wanajeshi wengine wanane wa Marekani na 11 wa Afghanistan wamejeruhiwa.

Kuuwawa kwa wanajeshi hao sita wa kunafanya jumla ya wanajeshi wa Marekani waliouwawa nchini Afghanistan kufikia 100 mwaka huu na kuufanya mwaka huu kuwa wa maafa makubwa kabisa kwa Marekani tokea kuvamiwa kwa nchi hiyo na mwaka 2001.