1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wapigana na waasi mashariki ya Chad

9 Mei 2009

Serikali ya Chad imesema kuwa hadi waasi 225 wameuawa katika mapigano ya siku mbili kati ya majeshi ya serikali na waasi hao.Vile vile wanajeshi 22 waliuawa katika mapigano hayo,mashariki ya nchi.

https://p.dw.com/p/HmWa

Tarakimu hizo lakini zimekanushwa na waasi wanaojaribu kuipindua serikali, tangu miaka mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa majeshi ya serikali yanapigana na vikosi vya waasi vinavyojongelea mji wa Abeche na mji mkuu Ndjamena.

Mapema juma hili,Chad na jirani Sudan zilitia saini makubaliano ya amani mjini Doha Qatar.Lakini sasa kila upande unamlaumu mwenzake kwenda kinyume na makubaliano hayo na kutoa msaada kwa waasi waliopania kupindua serikali za nchi hizo mbili.

Umoja wa Mataifa umearifu kuwa wafanyakazi wake 18 wamehamishwa kutoka eneo la mapigano na kuongezea kuwa kwa sababu ya mapigano hayo, itakuwa vigumu kutoa msaada kwa maelfu ya wakimbizi na wale waliopoteza makaazi yao.

Mwandishi: P.Martin-(AFPE)