1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi washangiriwa na kushukuriwa Bamako

28 Machi 2012

Maelfu ya watu wameandamana mjini Bamako leo kuunga mkono utawala wa kijeshi,siku sita baada ya wanajeshi hao kumpinduwa rais Amadou Toumani Touré.

https://p.dw.com/p/14TVF
Wannchi waandamana mjini BamakoPicha: AP

Waandamanaji wametaremka majiani kuunga mkono utawala wa kijeshi,siku ya pili tu baada ya tangazo la kubatilishwa sheria ya kutotoka nje saa za usiku,kupitishwa katiba mpya na kuahidi hakuna mwanajeshi yeyote atakaepigania wadhifa wowote serikalini,uchaguzi utakapoitishwa,tarehe ambayo bado haijulikani.

Waandamanaji wanaounga mkono utawala wa kijeshi wamebeba mabango na biramu zenye maandishi mfano "Hatumtaki ATT au Amadou Toumani Touré"Hatuitaki Ufaransa,"Htumtaki Sarkozy""umuia ya kimataifa isituingilie" na kadhalika.Mabango na biramu nyengine zinawasifu wanajeshi walionyakua madaraka mfano wa lile lililoandikwa :"Sanogo ndio ufumbuzi."

Waandamanaji wanadai wanajeshi wasalie madarakani ili kama wanavyosema kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kaskazini pamoja pia na yale yanayosiana na rushwa na elimu.

Alltag in Malis Hauptstadt Bamako
Maisha yanaanza kurejea kuwa ya kawaida mjini BamakoPicha: DW

Wakati wananchinyesha kuwaunga mkono nchini ,majirani na walimwengu kwa jumla wanawashinikiza wanajeshi warejeshe utawala unaoheshimu sheria.

Viongozi wa kijeshi wana mikakati yao.Kiongozi wao kepteni Amadou Sanogo anasema:"Kwakua yeye ni mwanajeshi, si mfuasi wa chama chochote cha kisiasa,wala si mwanasiasa ,kwa hivyo hana nia ya kushikilia wadhifa wa kisiasa.Anachopanga kufanya tena haraka,katika kipindi cha siku chache zijazo,kwanza ni kuhakikisha kundi lake linajulikana na pili kumteuwa waziri mkuu."

Shinikizo linazidi kukuwa dhidi ya viongozi hao wa kijeshi.Ujumbe wa wakuu wa vikosi vya wanajeshi wa jumuia ya nchi za Afrika magharibi umewasili Bamako kuandaa ziara ya ujumbe wa viongozi wa taifa na serikali wa jumuia hiyo unaoongozwa na rais Alassane Ouattara wa Côte d'Ivoire.Ujumbe huo wa marais sita huenda ukawasili kesho mjini Bamako kuzungumza na viongozi wa kijeshi kuhusu namna ya kurejesha nidhamu na kuheshimu katiba.

Hapo awali waziri wa mambo ya nchi za nje wa Bourkina Fasso,Djibril Bassolé aliiambia RFI kwamba viongozi wa jumuia ya ECOWAS wanapendelea kipindi cha mpito kiongozwe na spika wa bunge lililovunjwa na wanajeshi-Dioncounda Traore.

Navi Pillay
Navi Pillay-Mwenyekiti wa halmashauri ya Haki za binaadam ya Umoja wa mataifaPicha: picture alliance / dpa

Wakati huo huo mwenyekiti wa halmashauri ya haki za binaadam ya Umoja wa mataifa bibi Navi Pillay ameitolea mwito Mali iigize mfano wa Senegal na kuitisha uchaguzi huru na wa kidemokrasi kama ilivyokuwa ikifanya katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman