1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi zaidi wa UN wapelekwa kwenye kambi ya wakimbizi Rutshuru

7 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/EFQt

GOMA

Wanajeshi zaidi wa kuweka amani wa Umoja wa mataifa katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wamepelekwa kwenye kambi ya wakimbizi mashariki ya nchi hiyo ambako waasi wa Kihutu wa Rwanda wanadaiwa walifanya shambulio na kuua watu tisa.

Wanajeshi hao wataendelea kulinda eneo hilo ili kuzuia mashambulio zaidi dhidi ya wakimbizi.Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR waasi hao wakihutu wa kundi la FDLR jumatano walishambulia kambi ya Kinyandoni ilioko eneo la Rutshuru kaskazini mwa mji mwa mji wa Goma na kuua watu tisa.

Mashirika ya kutoa misaada yalisimamisha shughuli zao zote katika eneo hilo siku ya alhamisi kufuatia mashambulio ya waasi.