1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wa IS waandamwa na vikosi shirika vikisaidiwa na wakurd

1 Oktoba 2014

Nchi za ushirika unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la wanamgambo linalojiita Dola la Kiislamu, IS, zimefanya mashambulizi kaskazini ya Syria zikisaidiwa na vikosi vya Wakurdi katika mji wa Ain al-Arab

https://p.dw.com/p/1DOOK
Mapigano ya kuania mji wa Kobane nchini SyriaPicha: Reuters/Murad Sezer

Wanamgambo wa itikadi kali wa IS walikuwa umbali wa kilomita tatu tu mashariki ya mji huo ambao kwa kikurd unajulikana kama Kobané,karibu na mpaka na Uturuki-kwa mujibu wa shirika la Syria linalochunguza masuala ya haki za binaadam ,lenye mkao yake nchini Uingereza-shirika linalokusanya maelezo kutoka duru za kijamii,hospitali na pia kijeshi nchini Syria.

Ushirika wa Marekani na nchi za kiarabu" wamefanya hujuma zaidi ya mara tano dhidi ya vituo vya wanamgambo wa itikadi kali katika uwanja wa mapambano,mashariki na kusini mashariki ya Kobané-mkurugenzi wa shirika hilo la haki za binaadam la Syria Rami Abdel Rahmane ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Wanamgambo wasiopungua tisa wa IS wameuliwa,bomu lilipovurumishwa dhidi ya kifaru chao mashariki ya mji huo.Ingawa idadi yao ni ndogo na hawana silaha za kutosha,hata hivyo wapignaji wa kikurd wanapambana na wanamgambo wa itikadi kali wa IS wanaomiliki vifaru,silaha nzito nzito na makombora-shirika hilo la haki za binaadam linasema.

Wakurd wamepania kufa kupona kuuhami mji wa Kodane

Kwao wao hawajali kwasababu ni suala la kufa au kupona kuuhami mji wa Kobane" ameongeza kusema Rami Abdul Rahman.

Türkei - Syrische Flüchtlinge aus der Stadt Kobane
Wakimbizi wa Syria wanaouhama mji wa Kobane na kuingia UturukiPicha: Getty Images/Stringer

Wasiojiweza,wakinamma mwatoto na wazee wanaendelea kuuhama mji huo na kukimbilia Uturuki baada ya nchi hiyo kuacha wazi mipaka yake.

Wakurd wasiopungua laki moja na 60 elfu wameshaupa kisogo mji wa Kobane na vijiji vya karibu na hapo na kuingia Uturuki tangu septemba 25 iliyopita.Maelfu wengine wamekwama katika mji huo unaozingirwa kila upande na wanamgambo wa itikadi kali.

Anwar Moslem,ambae ni mkuu wa jimbo la Ain Al Arab anasema wanajaribu kukabiliana na wanamgambo wa itikadi kali wa IS kutokana na msaada wa hujuma za madege ya nchi shirika.

Wakurd wanakabiliana pia na wanamgambo wa IS nchini Iraq kutokna na msaada wa hujuma za madege ya Uingereza na Marekani dhidi ya wanamgambo hao wa itikadi kali.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vyapamba moto Syria

Wakati huo huo vita vya miaka mitatu na nusu vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vinaendelea kuangamiza maisha ya watu-watu 18 wameuwawa hii leo mabomu yaliporipuliwa ndani ya gari ktika mji unaodhibitiwa na serikali wa Homs.

Syrien - Anschlag in Homs
Bomu laripuliwa Karibu na shule huko HOms nchini SyriaPicha: Reuters

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/AFP

Mhariri: Mohammed Khelef