1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanariadha wajiandaa kutimka London marathon

11 Aprili 2014

Kikosi imara cha wanariadha nyota ikiwa ni pamoja na anayeshikilia rekodi ya ulimwengu Mkenya Wilson Kipsang na bingwa mara mbili wa Olimpiki Mo Farah kitashiriki katika mbio za London marathon Jumapili (13.04.14)

https://p.dw.com/p/1BgfJ
Leichtathletik WM Moskau Mo Farah
Picha: Reuters

Bingwa wa ulimwengu na Olimpiki Stephen Kiprotich, bingwa metetezi wa mbio za London Tsegaye Kebede na mwanariadha aliyeweka muda bora zaidi katika mbio za London marathon, Emannuel Mutai, pia ni miongoni mwa nyota watakaoshiriki huku pia Muethiopia Haile Gabreselassie akitarajiwa kuwapa motisha kwa kuongoza katika mstari wa mbele.

Macho hata hivyo yataangaziwa Farah mwenye umri wa miaka 31 anayetaka kuwa muingereza wa kwanza kushinda mbio za London marathon tangu Eamonn Martin katika mwaka wa 1993. Kama tu mwenzake Mo Farah, Katika mbio za wanawake, nyota Tirunesh Dibaba wa Ethiopia atajitosa kwa mara ya kwanza katika katika mbio za marathon.

Dibaba atafukuzana na bingwa mtetezi wa London Mkenya Priscah Jeptoo, na wakenya wenzake Ednah Kiplagat, bingwa wa sasa wa ulimwengu Florence Kiplagat anayeshikilia rekodi ya ulimwengu katika mbio za half marathon miongoni mwa wengine….Farah anasema anailenga rekodi ya kitaifa ya mwaka wa 1985 iliyowekwa na Steve Jones aliyetumia muda wa saa mbili dakika saba na sekunde 13.

Mshindi wa mbio za Berlin marathon Mkenya Wilson Kipsang Kiprotich atatoa upinzani mkali katika mbio za London
Mshindi wa mbio za Berlin marathon Mkenya Wilson Kipsang Kiprotich atatoa upinzani mkali LondonPicha: picture-alliance/dpa

Baadhi ya wapinzani wake wanaamini kuwa huenda ikawa vigumu kwa Farah kushiriki mbio kubwa kwa mara ya kwanza. Wakenya Kipsang na Mutai wanasema licha ya kwamba Farah anaweza kukimbia vyema, angestahili kuanza na mbio ndogo.

Mwezi mmoja uliopita, Farah alianguka na kuzirai baada ya kushinda mbio za New York marathon lakini anasisitiza yuko katika hali shwari. Kenenisa Bekele, ambaye baada ya kuutawala ulimwengu wa mbio za mita 5,000 na 10,000 alishiriki mbio zake za kwanza za marathon wikendi iliyopita mjini Paris na akashinda mbio hizo, jambo analosema hata Farah anaweza kufuata nyayo zake.

Tukisalia katika riadha, wmanariadha wa mbio za masafa mafupi Mjamaica Asafa Powell, ambaye aliwahi kushikilia rekodi ya ulimwengu yam bio za mita 100, ameishutumu hatua ya kupigwa marufuku ya miezi 18 akiitaja kuwa isiyokuwa ya haki.

Wakili wa mwanariadha huyo wamesema tayari watakata rufaa kuhusu hatua hiyo iliyofanywa na jopo la Jamaica la kinidhamu linalopambana na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni lenye wanachama watatu. Jopo hilo liliamuru wka kauli moja kuwa Powell, hastajili kushiriki mashindanoni baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu