1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake nchini Burkina faso

Omar Mutasa1 Juni 2007

Wanawake nchini Burkina faso wanadai na wao wapewe nyadhifa muhimu, katika kuendesha utawala bora wa nchi hio ya Burkina faso.

https://p.dw.com/p/CHDI
Mwanamke wa kibokinabe
Mwanamke wa kibokinabePicha: DW/Christine Harjes

Ni wanawake wachache ttu walioko kwenye Bunge la Burkina faso, ukilinganisha na idadi ya wabunge wanaume

Kutokana na madai ya muda mrefu wanawake wa Burkina faso wakitaka na wao alau wapewe nyadhifa muhimu katika Serekali hio,sasa kilio chao huenda kikasikika, kwani baadae mwaka huu Bunge la Burkina faso, litazungumzia sheria mpya ya kuwaongezea wanawake madaraka ya uongozi katika serekali hio.

Kuna wabunge 111 katika Bunge la Burkina faso, wabunge 13 wakiwa ni wanawake .

Mfumo wa uchaguzi wa Burkina faso aghlabu huwa vyama vya kisiasa hushinda viti bungeni kutokana na wingi wa kura zinazo- patikana kwa mgombea, hivo nyadhifa nono nono serekalini, hupewa wale wagombea waliopata kura nyingi.

Kuna zaidi ya vyama vya kisiasa 85 katika nchi hio ya Burkina faso ilioko Magharibi mwa bara la Afrika, na Rais wa kamati ya Bunge inayohusika na masuala ya haki za wanawake, Ousseni Tamboura anasema, ikiwa vyama vya kisiasa vitaachiwa uamuzi wa kupitisha maamuzi, basi hapatakueko

mwanamke katika baraza la Taifa . Ousseni Tamboura anaongeza kusema lazima pawepo mabadiliko yakisheria katika vyama vya kisiasa ili wanawake nao waweza kupewa madaraka ya nyadhifa za juu Serekalini.

Kamati hii ya bunge inayo husiana na wanawake kutoa maoni yao ya kisiasa iliundwa miaka miwili iliopita ikiwa na wabunge 27 .

Kulingana na Bi Mariam Sirima Afisa wa chama cha Muungano wa haki za wanawake

Wakibokinabe (Burkinabe Coalition of womens Rights ) anasema maoni ya mambo ya kitamaduni bado yanazuwia wanawake kupiga hatua mbele kisiasa, na bado wanaume wanaamini kua Siasa ni biashara yao.

Kwa mantiki hio ya wanaume, Bi Sirima anasema chama chao cha CBDF sasa kimeanza kuwailimisha wanawake katika mambo ya uongozi, pia kuboresha hali ya kuzungumza mbele ya hadhara ya watu, na pia kuwapa changa moto wanawake , ya kujihusisha na masuala ya kisiasa,ili waweze kupata nyadhifa za juu katika uchaguzi wa wabunge utakao fanyika tare sita May hapo mwakani.

Kwa sasa wanawake wa Burkina faso walioko bungeni wanafikia % 11.71 na azma yao wanataka kuona kwamba, wanawake wanafikia 30 % katika Bunge la Burkina faso.