1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake nchini Kenya wamenza kuvuka ukomo wa nafasi zao serikalini

13 Mei 2013

Wanawake nchini Kenye wanaanza kuvuka ukomo wa nafasi zao katika Serikali.Hii ni baada ya kuteuliwa wanawake 6 kati ya mawaziri 18 ambao wanaathibitishwa na kamati ya Bunge la Kenya.

https://p.dw.com/p/18X3c
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru KenyattaPicha: Getty Images

Idadi hiyo ya mawazri sita ilioteuliwa na serikali mpya ya Kenyatta ili kushika nafasi ya uwaziri kati ya mawaziri 18 wa nchi hiyo,inatajwa kuwa idadi ya juu sana nchini Kenya toka nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1963

Wanawake walioteuliwa ni pamoja na mwanadiplomasia wa zamani Raychelle Omamo,ambaye ameteuliwa kushika wizara nyeti ya ulinzi wizara ambayo haijawahi kushikwa na mwanamke katika historia ya nchi hiyo.

Mbali na huyo,mwanauchumi na mtaalamu wa sera za umma Anne Waiguru,naye kateuliwa kuongoza wizara muhimu ya mipango miji ambayo inaunganisha mfumo wa utakelezaji wa mipnago ya serikali mpya ya Kenya katika Kauti 47 .

Wengine ni Charity Ngilu,ambaye ameteuliwa kushika wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi,huku Phyllis Kandie,akiteuliwa wazriri wa biashara,utali na mambo ya Afrika Mashariki,na Judy Wakhungu,aliekuwa profesa katika chuo cha sayansi na tekenolojia chuo kikuu cha Pennsylvania,ameteuliwa kuongoza wizara ya Mazingira,Maji na mali asili.

Bado wanawake wachache katika utumishi wa umma

Mapema Aprili 23 mwaka huu Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na makamo wake William Ruto walitangaza kumteuwa Amina Mohamed kama mwanamke wa kwanza kuongoza wizara ya mambo ya nchi za nje,ambayo imekuwa ikiongozwa na wanaume 23 toka mwaka1963.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohamed
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina MohamedPicha: Getty Images

Kwa upande wake Maria Nzomo mwanamke wa kwanza nchini Kenya kupata shahada,ya uzamili ya sayansi ya siasa na masomo ya kimataiafa chuo kikuu cha Dalhousie nchini Canada mwaka 198,ameliambia shirika la habari la IPS, licha ya Uhuru Kenyatta kuteua wanawake katika nafasi hizo,lakini bado wanawake wengi wapo nyuma ya wanaume nchini Kenya.

Nzomo amesema kuwa wanawake wengi nchini humo wanaendelea kukabiliwa na changamoto ya kufikia huduma za afya,elimu na ushiriki wao katika nafasi za kisiasa,pamoja na ulinzi wa kisheria na vipaombele vingine katika uchumi.

Kwa sasa Nzomo,ambaye ni muhadhiri katika taasisi ya Kidiplomasia na masomo ya kimataiafa mjini Nairobi amesema serikali ya Kenya lazima ihakikisha inafanyia kazi changamoto za kijinsia zinazowakabili wanawake nchini Kenya

"Wanawake wanakosa ujuzi,elimu bora na utambuzi muhimu hii ikiwa inamaana wanawake wameonekana kutokuwa na faida kwa wanaume ambao wanaishi kwa kufanya kazi zisokuwa rasmi''amesema Nzoma,

Amesisitiza kuwa kuchagua wanawake hao sita kushika nafasi ya uaziri nchini Kenya isitafsiriwe kuwa ni kuwapa nafasi ya upendeleo kwa jinsia ya kike katika uaziri.

Sambamba na huyo,Grace Mbugua,mkurugenzi mkuu wa mtandao wa ajira kwa wanawake wa shirika la kitaiafa la haki za wanawake lisilokuwa la serikali ameliambia shirika la ahabari la IPS,kiwango cha nafasi za ajira kwa wanawake katika serikali ya Kenya kinatakiwa kuzidi zaidi ya hao wanwake sita walioteuliwa kuwa mawaziri.

"Lazima tusema tunakubali kuwa uongozi wa Rais Uhuru Kenyata,kwa kiasi umetekeleza matakwa ya kataiba ya Kenya mbali na hizo nafasi sita za wanawake katika sekta ya umma,lakini hii haina maana wanawake tunavuka kikomo chetu,bali serikali inatakiwa kuondoa utafauti wa kijinsia uliopo katika ya wanaume na wanawake nchini Kenya''amesema Grace Mbugua

Amesisitiza juu umuhimu wa usawa wa kijinsia kwamba serikali ya Kenya inatakiwa kutengeneza miundombinu muhimu ili kuondosha hali ya kutokuwa na usawa wa kijisia.

Hata hivyo amesema ili serikali ya Kenya ifanikiwe kuondoa utafauti wa kijinsia nchini humo,lazima serikali ihamasishe wanawake kushika uongozi kwa kuandaa sheria zitakazotumika katika uchaguzi ili kuwezesha wanawake kushiriki katika nafasi za kisasa.

Kupitishwa kwa mawaziri hao walioteuliwa katika kamati ya Bunge la Kenya,itakuwa imefikia kiwango cha theluthi moja ya jinsia ilioandaliwa katika katiba ya Kenya,licha ya kuwa idadi ya wanwake hao mawaziri haitoshi kumaliza utofauti wa kijinsia wakati nafasi nyingi za ajira katika serikali ya Kenya zinashikwa na jinsia ya kiume.

Ripoti ya mwaka ya maendeleo ya Benki ya Dunia ya mwaka inasema,juhudi za kuinnua wanawake katika nchi zinazoendelea kama Kenya haikupewa nafasi kwa muda mrefu,licha ya kuwapo na maendeleo kwa wanawake ya kujua haki zaoa na utafauti wa kijinsia.

Mwandishi:Hashim Gulana /IPS

Mhariri:Yusuf Saumu