1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina 2 wauawa Ukanda wa Gaza

19 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cugf

GAZA: Mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kijeshi za Israel leo alfajiri,kaskazini mwa mji wa Gaza, yameua si chini ya Wapalestina 2 wa chama cha Hamas.Madaktari wa Kipalestina wamesema,watu 4 wengine vile vile walijeruhiwa katika mashambulizi hayo.

Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi ya Israel,mashambulizi mawili ya angani kaskazini mwa Gaza,yalilenga vituo vinavyorusha makombora. Tangu siku ya Jumanne,zaidi ya Wapalestina 30 wameuawa katika mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.