1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani kushikiri mazungumzoya amani ya Syria

Sekione Kitojo
13 Februari 2017

Kundi kuu la upinzani nchini Syria liliidhinisha ujumbe mpya utakaoshiriki mazungumzo ya amani mjini Geneva yatakayofanyika baadaye  mwezi huu,yatakayo jumuisha makundi yanayoungwa mkono na Urusi.

https://p.dw.com/p/2XUGD
Kasachstan Syrien Friedensgespräche in Astana Opposition
Mkutano wa amani nchini Syria uliofanyika Astana KhazakhstanPicha: Reuters/M. Kholdorbekov

Hapo  kabla  makundi  hayo  yamekuwa  yakikosoa  makundi  yenye  silaha  kwa  kupambana  na  utawala  wa  rais bashar al-Assad.

Kamati  kuu  ya  majadiliano , HNC ikiwa  ni  chombo kinajumuisha  makundi  mengine  madogo  madogo , imesema  katika  taarifa  baada  ya  siku  mbili  za majadiliano  mjini  Riyadh  nchini  Saudi  Arabia , kwamba kikundi  hicho  chenye  wanachama  21 watakaoshiriki katika  majadiliano  ni  pamoja  na  makundi  wanachama mawili  ya  muungano  wa wapiganaji  ambao  hapo  kabla walikuwa  wanapingana.

Kasachstan Syrien Friedensgespräche in Astana Staffan de Mistura mit Mohammad Alloush
Mjumbe wa Umoja wa mataifa nchini Syria Staffan de Mistura (kulia) akiwa pamoja na Mohammad Alloush (kushoto)mkuu wa majadiliano wa zamani kwa upande wa upinzaniPicha: Getty Images/AFP/S. Filipov

Muungano  wa  makundi  hayo  mawili, lile  linalofahamika kama   makundi  ya  Moscow  na Cairo , kwa  muda  mrefu yamekuwa  yakipinga  mapigano  ya  waasi  na  kusisitiza kwamba  mabadiliko  ya  kisiasa  yanaweza  tu kupatikana kupitia  harakati  za  amani. Wanachama  wao  ni  pamoja na   waziri  wa  zamani  wa  serikali  ya  Syria  akiwa  na mahusiano  ya  karibu  na  Urusi.

Mohammad Sabra , ambaye  aliteuliwa  kuwa  mkuu  wa majadiliano, alikiambia  kituo  cha  televisheni kinachomilikiwa  na  Saudi Arabia  cha  Al-Hadath  kwamba ujumbe  huo  umeyaleta  pamoja  makundi  mbali  mbali.

Kasachstan Syrien Friedensgespräche in Astana
Mkutano wa kimataifa wa amani ya Syria mjini Astana nchini KhazakhstanPicha: Reuters/M. Kholdorbekov

Mataifa ya  kigeni 

Pia ameyashutumu  mataifa  ya kigeni yenye  nguvu ambayo  hakuyataja  kwa  kujaribu  kulazimisha  mawazo yao  juu  ya  muundo  wa  ujumbe  huo, akimaanisha Urusi.

Chombo  hicho  pia  kilimchagua  kiongozi  wao  mkuu mpya atakayeongoza  majadiliano, Nassir al-Hariri, mpinzani maarufu   akitokea  kusini  mwa  Syria.

Duru  ijayo  ya  mazungumzo  yanayosimamiwa  na  Umoja wa  Mataifa  kuhusiana  na  mzozo  huo, ukiwa  sasa  katika mwaka  wake  wa  sita , imepangwa  kuanza  Februari  20.

Kundi  la  HNC  limesema   katika  taarifa  kwamba  lengo la  majadiliano  hayo  ni  kupata  suluhisho  la  kisiasa  chini ya  usimamizi  wa  Umoja  wa  Mataifa   ambapo Assad hatakuwa  na  jukumu  katika  hatima  ya  nchi  hiyo. Lakini kundi  hilo  limejitoa  kutoka  katika  msimamo  wao  wa hapo  kabla  kwamba  rais  wa  Syria  analazimika kujiondoa  kabla  ya  kuanza  kwa   awamu  ya  mpito.

Syrien Interview Bashar al-Assad mit französischen Journalisten in Damaskus
Rais wa Syria Bashar al-AssadPicha: Reuters/Sana

Mswada  wa  katiba

HNC  pia  limesema  mataifa  ya  nje  yenye  nguvu hayana  haki  ya  kuweka  mtazamo  wao  kuhusiana  na mfumo  wa kisiasa  wa  hapo  baadaye  nchini  Syria. Urusi mwezi  uliopita  iliwasilisha  mswada  wa  katiba  mpya inayopendekezwa kwa  ajili  ya  Syria, licha  ya  kusisitiza kwamba  waraka  huo umesambazwa  kwa  madhumuni  ya majadiliano  tu.

Wakati huo  huo  serikali  ya  Syria  imesema  leo  kwamba iko  tayari  kukubaliana  kubadilishana  mateka  wa  vita , hatua  muhimu  ya  kujenga  hali  ya  kuaminiana  wakati Umoja  wa  Mataifa  ukijitayarisha  kuitisha  mazungumzo mapya  ya  amani.

Syrien Palmyra Tetrapylon
Mji wa kale wa PalmyraPicha: Getty Images/AFP/J. Eid

Upinzani  nchini  Syria  umekuwa  ukidai  kwa  muda  mrefu kuachiliwa  kwa  wafungwa  wanaoshikiliwa  na  serikali kama  moja  kati  ya  hatua  kadhaa  za  kibinadamu wanasema  ni  lazima  zifanyike  kabla  ya  majadiliano yoyote  kuhusiana  na  hali  ya  baadaye  ya   kisiasa nchini  Syria.

Nayo  majeshi  ya  Syria yamesogea  karibu  kilometa  20 kuelekea  mji  wa  Palmyra  katika  juhudi  za  kuukomboa mji  huo  wa  kale  kutoka  kwa kundi  la  waasi  la  Dola  la Kiislamu.

Mwandishi:  Sekione  Kitojo / rtre / dpae / afpe

Mhariri: Yusuf Saumu