1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani waandamwa Urusi

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CStr

Moscow:

Hatua kali zinaonyesha kuchukuliwa dhidi ya upande wa upinzani nchini Urusi,wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu kuitishwa.Mwanasiasa wa upande wa upinzani,bingwa wa zamani wa mchezo wa dama, Garri Kasparow amekamatwa na kuhukumiwa kifungo cha siku tano jela.Analaumiwa kuitisha maandamano,kinyume na sheria,dhidi ya rais Vladimr Putin.Garri Kasparov na wafuasi wa chama chake cha “Urusi Mpya” waliandamana kudai uchaguzi huru.Mbali na Kasparow,wapinzani wengine kadhaa wa serikali wamekamatwa.Mashahidi wanasema katika miji mengine pia polisi wamewakamata watu kwasababu ya kushiriki katika maandamano ya upande wa upinzani.