1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Warsaw.Maiti za mwisho katika migodi zapatikana.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqB

Wafanyakazi wa huduma za uokozi kusini mwa Poland wameigundua miili mingine miwili iliyokuwa haionekani, baada ya hapo jana kuripuka kwa mgodi.

Kugunduliwa kwa miili hiyo kunaifanya idadi ya mwisho ya waliofariki kutokana na maafa hayo kuongezeka na kufikia 23.

Msako wa wachimba maadini kwa siku mbili zilizopita ulikuwa umezorota kutokana na khofu ya kuzuka kwa mripuko mwengine, kulikosababishwa na ongezeko la gesi ya Methane.

Maafisa wa uokoaji wamesema, hawawezi kuelezea ikiwa wafanyakazi hao walikufa kwa namna gani.