1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WARSAW:Poland kusaidia juhudi za kufufua katiba ya Umoja wa Ulaya

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCI0

Rais wa Poland Lech Kaczynski amemwambia Kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel kuwa Poland haitazuia juhudi za kufufua katiba ya Umoja wa Ulaya.

Bwana Kaczynski ameeleza kuwa nchi yake inakubaliana na Ujerumani juu ya kuanzisha tena mazungumzo juu ya katiba hiyo katika msingi wa maudhui ya sasa. Katiba ya Umoja wa Ulaya, imeidhinishwa na nchi 18 za Umoja huo lakini ilikataliwa katika kura za maoni zilizofanyika nchini Ufaransa na Uholanzi mnamo mwaka wa 2005.

Wakati huo huo Kansela Angela Merkel amemaliza ziara ya siku mbili nchini Poland ambapo pia alizungumza na wenyeji wake juu ya mpango wa Marekani wa kuweka kituo cha ulinzi dhidi ya makombora nchini humo.