1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Warusi wapiga kura

Sekione Kitojo
18 Machi 2018

Warusi wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa rais Jumapili (18.03.2018) unaotarajiwa kumpa Putin ushindi mkubwa ambao unaweza tu kuchafuliwa iwapo watu wengi hawatajitokeza kupiga kura kwa sababu matokeo yanatabirika.

https://p.dw.com/p/2uXIh
Präsidentenwahl in Russland  Wahllokal
Picha: picture-alliance/AP/A. Petrov

Katika eneo  la  mashariki  mwa  Urusi, katika  mji  wa  pwani  ya  bahari  ya  Pacific wa Petropavlovsk-Kamchatsky, vituo  vya  kupigia  kura  vilifunguliwa  mapema saa  tano usiku saa  za  Urusi, na  upigaji  kura utaendelea  katika  nchi  hiyo  kubwa  hadi  vituo vitakapofungwa  katika  eneo  la  magharibi  kabisa  mwa  nchi  hiyo katika  jimbo  la Kaliningrad , masaa  22  baadaye.

Russland Präsidentschaftswahlen Nordwestrussland Nenzen
Mfugaji akipiga kura yake katika maeneo ya mbali nchini Urusi.Picha: Reuters/S. Karpukhin

Uchunguzi  wa maoni  ya  wapiga  kura  unampa Putin , rais  wa  sasa , uungwaji  mkono  wa kiasi  ya  asilimia  70, ama  karibu  mara  10  zaidi ya uungwaji  mkono  wa  mgombea anayemkaribia. Muhula  mwingine  utamchukua karibu  robo  karne  akiwa  madarakani, muda  mrefu  zaidi  miongoni  mwa  viongozi  wa  serikali  ya  Kremlin wapi  tu kwa  dikteta wa  enzi  wa  Kisovieti Josef Stalin.

Wengi  wa  wapiga  kura  wanamsifu  Putin, mwenye  umri  wa  miaka  65 jasusi  wa  zamani wa shirika  la  kijasusi  la  Urusi , KGB, kwa  kutetea  masilahi  ya  Urusi katika  dunia  hii yenye  uhasama, hata  kama  gharama  ni  mapambano  dhidi  ya  mataifa  ya  magharibi.

Mzozo  na  Uingereza  kuhusiana  na madai  kwamba  Kremlin ilitumia  sumu inayoathiri mishipa  ya  fahamu dhidi  ya  jasusi  wa  zamani  wa  Urusi  katika  mji mtulivu  wa  Uingereza , madai  ambayo  Urusi  inakana , haujachafua  uungwaji  wake  mkono.

Wengi  wa  wapiga  kura  hawaoni mtu mbadala  kwa  Putin, ana udhibiti  kamili  wa  medani ya  kisiasa  pamoja  na  televisheni  ya  taifa, ambako watu  wengi wanapata  taarifa  zao, na kutoa muda  mkubwa  kwa  matangazo yanayomhusu  Putin na  muda  mchache  kwa wagombea  wengine.

Präsidentenwahl in Russland Wahllokal
Wapiga kura wakipiga kura katika uchaguzi wa rais nchini Urusi Picha: picture-alliance/AP/A. Petrov

"Putin ndio rais  wetu. Tunajivunia," amesema  Marianna Shanina, mkaazi wa  jimbo  la Crimea. Urusi  ililinyakua  jimbo  la  Crimea  kutoka  Ukraine miaka  minne  iliyopita, na kumpa  sifa  Putin kutoka  kwa  Warusi  wengi  na  shutuma  kutoka  mataifa  ya  magharibi.

Warusi hawana mbadala kwa Putin

"Tunamtakia  ushindi  katika  uchaguzi. Familia  yetu  yote itampigia  kura Putin. Putin ! Afya njema  kwako, rais wetu  mpenzi !," Shanina  alisema  katika  mkutano  wa  kampeni  wa Putin.

Uchunguzi  wa  maoni  ya  wapiga  kura  uliofanywa  Machi 9  na  kampuni  inayomilikiwa  na serikali  ya  VTsIOM ilimpa Putin ambaye  alichaguliwa  mara  ya  kwanza  kuwa  rais  mwaka 2000, uungaji  mkono  wa  asilimia  69. Mgombea  aliyeko  karibu  nae Pavel Grudinin , mgombea  wa  chama  cha  Kikomunist , atapata  asilimia  7.

Wahlen Russland 2018 - Wahlstation - Kandidatenliste
Mjumbe wa tume ya uchaguzi nchini Urusi akiweka karatasi inayoonesha picha za wagombea katika uchaguzi nchini UrusiPicha: Getty Images/AFP

Mwanasiasa  wa  kwanza katika  miaka  kadhaa  kutoa changamoto  kwa  udhibiti  wa serikali  madarakani, Alexei Navalny, amezuiwa  kushiriki  katika  uchaguzi  huo  kwasababu ya  kuhumumiwa  kwa  madai  ya  rushwa, madai  ambayo  anasema  alibambikiwa na serikali.

Anatoa  wito  wa  kuususia  uchaguzi  huo, akisema  ni  kichekesho cha  kitokuwa  na demokasia, na kuwaweka  waungaji  wake  mkono  kukusanya  ushahidi  wa  mtu  yeyote atakayefanya  udanganyifu  katika  uchaguzi  kuweka  idadi  ya  juu  ya  watu  watakaoshiriki katika  uchaguzi  huo  na  uungwaji  mkono  wa  Putin.

Russland Wahlen - Alexei Navalny wird festgenommen
Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny ambaye amezuiwa kugombea katika uchaguzi huo akikamatwa na poilisi, Januari 28, 2018Picha: picture alliance/AP Photo/E. Feldman

Serikali  ya  Urusi pembeni  inakiri  kuwa  na  wasi  wasi kwamba  baadhi  ya   Warusi  milioni 110  wenye  haki  ya  kupiga  kura  hawatajisumbua  kupiga  kura  kwasababu  wanaamini Putin  atashinda  tu.  Uchache  wa  watu  watakaojitokeza  kupiga  kura  utaathiri  mamlaka yake  katika  muhula  ujao, ambao , chini  ya  katiba, utakuwa  wa  mwisho.

Katika  hotuba kwa  taifa  iliyotangazwa  moja  kwa  moja  na  televisheni  ya  taifa  siku  ya Ijumaa, Putin  alisema  wapigakura  wana mustakabali  wa  nchi  hiyo  katika  mikono  yao.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Yusra Buwayhid