1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasanii wa Kenya waonyesha umahiri wao

Reuben Kyama24 Julai 2015

Wasanii nchini Kenya wanaitumia ziara ya Barack Obama kuonyesha namna walivyo wabunifu. Reuben Kyama amekutana na mmoja wao jijini Nairobi ili kuona akazi zake na kufahamu zaidi kuhusu biashara yake.

https://p.dw.com/p/1G3zK
Fulana za Obama Nairobi
Picha: DW/R. Kyama

Huku shamrashamra za kumlaki Rais wa Marekani Barack Obama zikishika kasi nchini Kenya, baadhi ya wasanii na wafanyabiashara jijini Nairobi na kwengineko nchini humo tayari wamebuni njia mbalimbali za kuwavutia wateja kwa kusudi la kufanya biashara kabambe wakati wa ziara ya Rais huyo katika taifa hilo la Afrika ya Mashariki.

Mwandishi wetu Reuben Kyama amekutana na Mark Madegwa, mkazi wa mtaa wa mabanda wa Kibera jijini Nairobi. Yeye ni moja wa wasanii wanaojikaza kisabuni kuona kuwa wametumia nafasi hii ili kuonyesha ustadi wao katika uwanja wa uchoraji pamoja na kukuza mauzo ya biashara zao wakati wa ziara ya Kiongozi huyo wa Marekani nchini humo.

Kusikiliza mahojiano bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.