1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Baraza la wawakilishi laidhinisha malipo ya fidia kwa wafiwa.

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKe

Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani limepiga kura jana kuwalipa fidia familia za Wamarekani 12 waliouwawa katika shambulio linalohusiana na kundi la kigaidi la al-Qaeda dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya mwaka 1998. Chini ya muswada huo wa sheria uliopitishwa kwa kura 409 dhidi ya 12, kila familia itapata kiasi cha dola 940,000.

Muswada huo wa sheria sasa utapelekwa katika baraza la Seneti.

Kama familia zilizoathirika na shambulio la Septemba 11, familia za watu waliouwawa katika shambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi pia wameathirika na mashambulizi ya kundi la Al-Qaeda, amesema mbunge wa baraza la wawakilishi kutoka chama cha Democratic Jesse Jackson Jr, ambaye amedhamini muswada huo pamoja na mbunge wa baraza hilo kutoka chama cha Republican Roy Blunt.