1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Baraza la wawakilishi laweka muda wa kuondoa majeshi.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6r

Baraza la wawakilishi la Marekani limeidhinisha muswada wa kuhudumia vita wenye thamani ya dola bilioni 100 kwa ajili ya Iraq na Afghanistan , lakini limeweka muda wa majeshi yote ya Marekani kuondoka nchini Iraq ifikapo March 31 mwaka ujao.

Baraza hilo linalodhibitiwa na chama cha Democratic limepiga kura 218 dhidi ya 208 kukubali muswada huo, wakikaidi vitisho vya rais George W. Bush ambaye ametishia kupiga kura ya turufu dhidi ya mpango wowote utakaohusisha muda wa kuyaondoa majeshi.

Wademocrats wameimarika kutokana na uchunguzi mpya wa maoni unaoonyesha kuwa asilimia 56 ya Wamarekani wanataka muda maalum.

Kabla ya baraza hilo kupiga kura , kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Iraq David Petraeus aliwahutubia wabunge mjini Washington. Amesema kuwa kumekuwa na maendeleo katika kupunguza mauaji ya kimadhehebu mjini Baghdad. Baraza la Seneti , linapiga kura leo kuhusu muswada huo.