1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush amekiri makosa katika sera ya Irak

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuP

Rais George W.Bush wa Marekani,anapaswa kujirekebisha na hali mpya iliyozuka kufuatia uchaguzi wa bunge,kuwa chama chake cha Republikan hakina tena uwingi katika mabaraza yote mawili ya bunge.Kwani kwa mujibu wa vyombo vya habari,chama cha upinzani cha Demokrat,kimejinyakulia ushindi katika Seneti pia.Tangu siku ya Jumatano ilidhihirika kuwa Wademokrats nchini Marekani kwa mara ya kwanza,baada ya miaka 12 watakuwa na wajumbe wengi zaidi katika Baraza la wawakilishi.Baada ya pigo hilo la uchaguzi,rais Bush amekiri makosa katika sera za serikali yake kuhusu Irak.Wakati huo huo alitangaza kuwa waziri wa ulinzi Donald Rumsfeld amejiuzulu kutokana na kushindwa kwa chama cha Republikan.Robert Gates ambae hapo zamani alikuwa mkurugenzi wa idara ya upelelezi ya Marekani-CIA anatazamiwa kumrithi Rumsfeld katika Pentagon.