1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush amteua rais mpya wa benki kuu ya dunia.

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwn

Afisa mwandamizi katika serikali ya Marekani amesema kuwa rais George W. Bush amemchagua Robert Zoellick, mwakilishi wa zamani wa biashara wa nchi hiyo, kuwa rais mpya wa benki ya dunia.

Afisa huyo ameongeza kuwa Bush anapanga kutangaza uteuzi wake huo leo Jumatano na anatarajia bodi ya benki hiyo itamkubali.

Kwa kawaida rais wa benki hiyo hutoka Marekani licha ya kuwa kumekuwa na miito kadha kila mara kuiweka nafasi hiyo wazi kwa watu kutoka mataifa mengine , kufuatia kuondoka kwa rais wa sasa Paul Wolfowitz.

Zoellick aliwahi kuwa afisa katika wizara ya mambo ya kigeni nchini Marekani hadi alipoacha kazi serikalini mwaka jana na kujiunga na benki ya rasilimali ya Goldman Sachs.