1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush apiga marufuku mateso ya wafungwa

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgX

Rais George W. Bush wa Marekani amepiga marufuku matumuzi ya mateso wakati wa kuwahoji wanaoshukiwa ugaidi.Bush amechukua hatua hiyo kutokana na shinikizo la Mahakama Kuu ya Marekani.Amri hiyo inapiga marufuku vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wafungwa.Serikali ya Marekani kwa kutoa amri hiyo,inataka kutekeleza masharti ya Mktaba wa Geneva unaozuia kuwatesa wafungwa.Lakini makundi yanayogombea haki za binadamu yanasema,Bush hajapiga marufuku baadhi ya vitendo,kama vile kuwanyima wafungwa usingizi au kufanya kama kutaka kuwazamisha.Bush, ameshinikizwa nyumbani na nchi za ngámbo,kuhusika na vile washukiwa wanavyotendewa katika jela za siri za shirika la ujasusi la Marekani CIA,ikiwa ni pamoja na jela ya Guantanamo Bay na pia wakati wa kufanywa safari za ndege za kuingia na kutoka kwa siri,nchi za Ulaya.