1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush atetea sera za vita vya Irak

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBib

Rais George W.Bush wa Marekani kwa mara nyingine tena amejitetea dhidi ya wakosoaji wa sera za serikali yake nchini Irak.Bush amekiri kuwa ripoti iliyotolewa juma hili imesema kuwa serikali ya Irak imeshindwa kutekeleza mageuzi muhimu kuhusu masuala manane mbali mbali,lakini vile vile imeridhisha katika mambo manane mengine.Kwa hivyo amesema,kuna sababu ya kuwa na matumaini.

Bush akaeleza kwamba msingi wa mkakati ni kuwa maendeleo ya usalama yatafungua njia ya kuleta maendeleo ya kisiasa.Ripoti yaonyesha kuwa masharti yaweza kubadilika,maendeleo yanaweza kupatikana na vita vya Iraq lazima vipate ushindi.