1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush kumchagua mrithi wa Wolfowitz

22 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzh

Ikulu ya Marekani imearifu kuwa Rais George W. Bush anapanga kumteua raia wa Kimarekani kuchukua nafasi ya Paul Wolfowitz kama rais wa Benki ya Dunia.Kuambatana na makubaliano ya kimataifa,rais wa Marekani,ndie anaechagua mkuu wa Benki ya Dunia.Juma lililopita,Wolfowitz alikubali kuondoka madarakani mwisho wa mwezi ujao.Kiongozi huyo wa benki alishinikizwa na jumuiya ya kimatafa ajiuzulu,baada ya kujulikana kuwa muda mfupi tu baada ya kuingia katika Benki ya Dunia, alimpandisha cheo mpenzi wake na kumpa nyongeza kubwa ya mshahara.