1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON. Condoleeza Rice azungumza na Hamas !

18 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC99

Kwa mara ya kwanza , waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice amekutana na waziri wa serikali ya wapalestina inayoongozwa na chama cha Hamas.

Waziri Rice alishiriki kwenye mazungumzo yaliyofanyika baina ya naibu wake bwana David Welch na waziri wa fedha wa Palestina bwana Salam Fayyad .Hakuna habari zaidi juu ya mazungumzo hayo.

Hadi hivi karibuni Marekani ilikuwa inakataa kuwasiliana na wajumbe wa Hamas.