1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Condoleezze Rice atazamiwa Mashariki ya Kati

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRi

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,Condoleezza Rice,anatazamiwa kuwasili Mashariki ya Kati mwishoni mwa juma hili kwa matayarisho ya mkutano wa kilele pamoja na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas. Rice amepanga kukutana na waziri wa masuala ya nje wa Israel,Tzipi Livni,Jumamosi usiku,.Vile vile siku ya Jumapili,atakuwa na mikutano mbali mbali na Olmert na Abbas katika miji ya Jerusalem na Ramallah.Azma ya majadiliano hayo ni kutayarisha mkutano wa kilele wa pande tatu unaotazamiwa kufanywa siku ya Jumatatu.