1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Kansela Merkel na rais Bush wakubaliana kutumia diplomasia kuumaliza mzozo wa nyuklia wa Iran

11 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJx

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel na rais wa Marekani George W Bush wamekubaliana kutumia diplomasia kuumaliza mzozo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Rais Bush ameipongeza Ujerumani kwa juhudi zake nchini Irak. ´Kwa kuwa sasa demoksrasia mpya nchini Irak inachipuka natambua mchango wa Ujerumani na anashukuru kwamba serikali ya Ujerumani insaidia kutoa mafunzo kwa polisi nchini Irak.´

Kansela Merkel amewaambia waandishi wa habari alipokuwa nyumbani kwa rais Bush katika jimbo la Texas kwamba Ujerumani huenda ikaunga mkono awamu nyingine ya vikwazo dhidi ya Iran ikiwa nchi hiyo itaendelea kuipuuza jumuiya ya kimataifa.

Kansela Merkel amesema, ´Ikiwa mazungumzo kati ya mjumbe wa Iran na mjumbe wa Umoja wa Ulaya bwana Javier Soalana hayataulu, na ikiwa ripoti ya shirika la kimatiafa la kuzuia usambazaji wa silaha za kinyuklia haitaridhisha, ipo haja ya kufikiria kuiwekea Iran vikwazo vipya.´

Wakati wa ziara yake iliyodumu muda wa saa 20, kansela Merkel alieleza juu ya azma ya serikali ya mjini Berlin kutaka kiti cha kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, lakini rais Bush hakusema ikiwa ataliunga mkono pendekezo hilo.

Kansela Merkle pia hakuwa na bahati ya kuungwa mkono alipoitaka Marekani ipunguze gesi za viwandani zinazoharibu mazingira.

Rais Bush amesema anafahamu tatizo hilo lipo lakini juhudi za kuilinda hali ya hewa haziwezi kuruhusiwa kuvuruga uchumi.