1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Kesi za wafungwa wa Guantanamo haziwezi kusikilizwa na mahakama za majimbo

21 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQ6

Mahakama ya Marekani imeamua kwamba wafungwa wa jela ya Guantanao Bay nchini Cuba hawawezi kuwasilisha mashtaka ya kuzuiliwa kwao katika jela hiyo kwenye mahakama za majimbo.

Mahakama ya rufaa mjini Washington imeamua kwamba mahakama hizo hazina mamlaka kusikiliza kesi za wafungwa wanaozuiliwa katika jela ya Guantanamo.

Uamuzi huo unaheshimu sheria ya tume ya jeshi iliyoidhinishwa na bunge la Congress na kutiwa saini na rais George W Bush wa Marekani mnamo mwaka jana.