1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON :: Liberia kufutiwa madeni.

13 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJT

Shirika la fedha la kimataifa IMF limesema lipo tayari kuifutia deni Liberia baada ya nchi kadhaa kuahidi kutoa kiasi cha dola milioni mia 8 na 42 .

Mkurugenzi wa shirika la IMF bwana Domique Strauss Khan amesema hatua hiyo ni muhimu sana kwa Liberia nchi ambayo sasa inajijenga upya baada vita vya miaka 14.

Watu zaidi ya laki 2 na alfu 70 walikufa katika vita hivyo vilivyomalizika mnamo mwaka 2003.

Liberia imekuwa inakabiliwa na ugumu katika kutafuta mikopo kutokana na deni linalokadiriwa kufikia dola bilioni 4 na nusu.