1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mahakama kuu kutolazimika kuamua kesi za Guantanamo

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCz

Mahakama kuu nchini Marekani imepitisha uamuzi kuwa haitalazimika kufanya maamuzi kuhusu iwapo watuhumiwa wanaozuiliwa katika jela ya Guantanamo Bay wana haki ya kupinga kuzuiliwa kwao.

Uamuzi huo ni kama kupigwa kofi utawala wa rais Bush kwani mahakama kuu sasa haitalazimika kutoa uamuzi kuhusu kipengele katika pendekezo la katiba la rais Bush kuhusu sheria za kupambana na ugaidi.

Kipengele hicho kilikuwa kinawazuia watuhumiwa kuomba kesi zao zisikilizwe katika mahakama za kisheria nchini Marekani na badala yake pendekezo hilo liliundwa ndani ya katiba na kuzipa uwezo mahakama za kijeshi kushughulikia kesi za watuhumiwa wa ugaidi.

Zaidi ya watuhumiwa 400 katika jela ya Guantanamo Bay wamezuiliwa hadi kufikia miaka mitano.