1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yalenga kuhifadhi mipaka ya Irak

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQN

Waziri wa masuala ya nje wa Marekani,Condoleezza Rice amesema,Marekani italenga kuhifadhi mipaka ya Irak.Alitamka hayo baada ya Iran kuonya kuwa itaziba pengo litakaloachwa,baada ya majeshi ya Marekani kuondoka Irak.Hapo awali,serikali ya Irak ilisema,idadi ya wanajeshi wa Kimarekani nchini Irak mwishoni mwa mwaka 2008,inatazamiwa kupunguka hadi 100,000 kutoka jumla ya wanajeshi 168,000 waliopo hivi sasa nchini humo.