1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yataka vikwazo vipya dhidi ya Sudan

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBx2

Marekani inapanga kuiwekea Sudan vikwazo vipya kuhusika na mgogoro wa Darfur na baadae katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa itapendekeza azimio jipya lililo kali zaidi. Katika orodha ya vikwazo vipya,inatazamiwa kuwa hatua hizo zitalenga makampuni ya mafuta yanayomilikiwa au kudhibitiwa na serikali ya Sudan.Mapigano kati ya wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali ya Kahartoum na makundi ya waasi kwenye jimbo la Darfur,magharibi mwa Sudan yameua zaidi ya watu 200,000 na wengine wapatao kama milioni 2 wamelazimika kukimbia makwao.