1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mpango wa Marekani usifananishwe na mzozo wa Kuba

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CG

Serikali ya Marekani imepinga kufananishwa kwa mpango wa Marekani kuweka makombora ya kujihami katika Ulaya ya Mashariki na ule mzozo wa Kuba wa mwaka 1962.Marekani inasema,lengo la mradi wake wa kutaka kuweka makombora ya kinga nchini Poland na Jamhuri ya Czech,ni kujihami dhidi ya mashambulizi ya makombora,kutoka nchi za ukorofi kama vile Iran.

Mradi huo umesababisha mvutano katika uhusiano wa Urusi na Marekani.Rais wa Urusi,Vladimir Putin anaupinga mradi huo na amefananisha mgogoro wa sasa na ule wa mwaka 1962 kati ya Marekani na Soviet Union ya zamani.Wakati huo,kulizuka hatari ya kutokea vita vya nyuklia kati ya madola hayo mawili makuu.