1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mshukiwa amekiri kupanga shambulizi la Septemba 11

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIc

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema,kiongozi mmojawapo mkuu wa Al Qaeda,Khalid Sheikh Mohamed amekiri kupanga mashambulizi 31 ya kigaidi yaliyoafanywa sehemu mbali mbali duniani.Miongoni mwa mashambulizi hayo ni yale ya Septemba 11 mwaka 2001.Inasemekana kuwa alikiri hayo mbele ya mahakama ya kijeshi katika kambi ya wafungwa ya Guantanamo Bay inayoongozwa na Marekani.Sehemu ya nakala ya makosa aliyokiri katika kikao cha faragha,ilitolewa na wizara ya ulinzi-Pentagon. Humo,Mohammed alidai kuwa alihusika na mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia pamoja na mauaji ya muandishi wa habari wa Kimarekani,Daniel Pearl nchini Pakistan.