1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Mtuhumiwa akiri kupanga mashambulizi.

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIv

Mtuhumiwa mkuu na anayeshukiwa kuwa ndie aliyepanga njama za mashambulizi ya kigaidi ya hapo Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani , anaripotiwa kukiri kupanga mashambulizi hayo.

Khalid Sheikh Mohammed anasemekana kutoa maelezo hayo katika kikao cha faragha katika jela ya Guantanamo Bay.

Katika maelezo yake, Mohammed amesema kuwa anahusika na operesheni yote pamoja na matukio mengine yanayohusiana na mtandao wa kigaidi wa Al Qeda. Kwa jumla , Mohammed amesema amepanga jumla ya mashambulizi 29 ikiwa ni pamoja na jaribio lililofanywa na anayejulikana kama mshambuliaji wa bomu la kiatu Richard Reid dhidi ya ndege ya abiria.