1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mwanasheria mkuu wa Marekani ajiuzulu

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVM

Mwanasheria mkuu wa Marekani Alberto Gonzales amejiuzulu baada ya kipindi cha kashfa kilichougubika utumishi wake katika wadhifa huo.

Maafisa wa wizara ya sheria hawakupatikana kwa haraka kuweza kutoa hisia zao kuhusiana na kujiuzulu kwa Albetro Gonzales.

Gonzales, mfuasi wa rais George W Bush mwenye umri wa miaka 51, alikuwa kitovu cha mabadíliko ya kisiasa ya rais Bush katika kashfa ya kufutwa kazi waongazaji mashataka wanane wa serikali.

Wakosoaji wengi katika bunge la Marekani walisema kufutwa kazi maafisa hao kulichochewa kisiasa.

Gonzales alimwambia rais Bush Ijumaa iliyopita kwamba angejiuzulu na kwamba nafasi yake haitakuwa wazi kwa muda mrefu.

Alberto Gonzales alifanya kazi na rais Bush kwa mara ya kwanza alipokuwa gavana wa jimbo la Texas katika miaka 1990.

Alifanya kazi kama wakili wa ikulu ya Marekani wakati wa awamu ya kwanza ya rais Bush kabla kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Uhispania mnamo mwezi Februari mwaka wa 2005.