1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Nchi za Ghuba kusaidiwa kijeshi na Marekani

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeU

Marekani inafanya mpango wa kuziimarisha kijeshi Saudi Arabia na nchi zingine tano za Ghuba.Kwa mujibu wa gazeti la „Washington Post“ katika kipindi cha miaka kumi ijayo,nchi hizo za Mashariki ya Kati zitauziwa silaha za kisasa kabisa ikiwa ni pamoja na makombora ya anga na manowari mpya.Biashara hiyo ina thamani ya Dola bilioni 20.Azma ya mpango huo ni kuimarisha madola shirika ya Marekani na vile vile kupambana na ushawishi wa Iran unaozidi kuenea katika kanda hiyo.Mbali na nchi hizo za Ghuba,msaada mwingine wa Dola bilioni 43 utatolewa na Marekani kwa ajili ya Israel na Misri.